Biblia ya King James Version
Waefeso, Sura ya 1:
- Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, kwa watakatifu walioko Efeso, na waaminio katika Kristo Yesu;
- Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
- Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
- kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika upendo;
- akiisha kutuchagua tangu asili, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake;
- Kwa sifa ya utukufu wa neema yake, ambayo ametufanya tukubalike ndani yake huyo mpendwa.
- Ambaye katika yeye tuna ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake;
- Naye ametuzidishia katika hekima yote na busara;
- akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake mwema, alioukusudia ndani yake.
- Ili katika kipindi cha utimilifu wa nyakati avikusanye pamoja vitu vyote katika Kristo, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi pia; hata ndani yake:
- Ambaye katika yeye sisi nasi tumepata urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake mwenyewe.
- Ili tuwe kwa sifa ya utukufu wake, ambao kwanza tulimtumaini Kristo.
- Nanyi pia katika yeye mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu;
- ambayo ndiyo arabuni ya urithi wetu mpaka ukombozi wa milki yetu, kuwa sifa ya utukufu wake.
- Kwa sababu hiyo mimi nami, niliposikia juu ya imani yenu katika Bwana Yesu, na upendo wenu kwa watakatifu wote;
- Siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu, nikiwataja katika maombi yangu;
- Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;
- Macho ya akili yako yatiwe nuru; mpate kujua tumaini la mwito wake jinsi lilivyo, na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;
- Na ukuu wa ukuu wa uweza wake kwetu sisi tuaminio jinsi ulivyo, kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake mkuu;
- Aliyoyatenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;
- juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali katika ule ujao pia;
- akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa;
- ambao ni mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.