Biblia ya King James Version
Yohana, Sura ya 1:
- Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
- Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
- Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
- Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima; na huo uzima ulikuwa nuru ya watu.
- Nayo nuru yang’aa gizani; wala giza halikuiweza.
- Palikuwa na mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana.
- Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile Nuru, watu wote wapate kuamini kwa yeye.
- Yeye hakuwa ile nuru, bali alikuja kushuhudia ile nuru.
- Hiyo ndiyo nuru halisi, ambayo huwaangazia kila mtu ajaye ulimwenguni.
- Alikuwako ulimwenguni, na kwa yeye ulimwengu uliumbwa, wala ulimwengu haukumtambua.
- Alikuja kwa walio wake, na walio wake hawakumpokea.
- Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
- Waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
- Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.
- Yohana alishuhudia habari zake, akapaza sauti yake akisema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu mkuu kuliko mimi, kwa maana alikuwa kabla yangu.
- Na katika utimilifu wake sisi sote tumepokea, na neema juu ya neema.
- Kwa maana torati ilitolewa kwa mkono wa Musa, bali neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
- Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote, Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.
- Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?
- Naye alikiri, wala hakukana; lakini alikiri, Mimi siye Kristo.
- Wakamwuliza, Je! Je, wewe ni Eliya? Akasema, Si mimi. Wewe ni nabii yule? Naye akajibu, La.
- Basi wakamwambia, Wewe ni nani? ili tupate kuwajibu wale waliotutuma. Unasema nini juu yako mwenyewe?
- Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana, kama alivyosema nabii Isaya.
- Na wale waliotumwa walikuwa wa Mafarisayo.
- Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala yule nabii?
- Yohana akawajibu, akasema, Mimi nabatiza kwa maji;
- Yeye ndiye ajaye baada yangu, ambaye mimi sistahili hata kuilegeza gidamu ya kiatu chake.
- Mambo hayo yalifanyika huko Bethania, ng’ambo ya mto Yordani, mahali Yohana alipokuwa akibatiza.
- Siku ya pili yake akamwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.
- Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Baada yangu anakuja mtu ambaye amekuwa mbele yangu kwa maana alikuwa kabla yangu.
- Wala mimi sikumjua, lakini mimi nalikuja nikibatiza kwa maji ili adhihirishwe kwa Israeli.
- Naye Yohana alishuhudia akisema, Nilimwona Roho akishuka kama njiwa kutoka mbinguni, akakaa juu yake.
- Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenituma kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yule utakayemwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.
- Nami nimeona na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.
- Kesho yake tena Yohane alikuwa amesimama pamoja na wanafunzi wake wawili;
- Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu!
- Wanafunzi wawili wakamsikia akisema, wakamfuata Yesu.
- Yesu akageuka, akawaona wanamfuata, akawauliza, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (yaani, Mwalimu), unakaa wapi?
- Akawaambia, Njoni mwone. Wakaenda, wakaona mahali alipokuwa anakaa, wakakaa naye siku hiyo, kwa maana ilikuwa yapata saa kumi.
- Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohane akisema hivyo, wakamfuata Yesu.
- Huyo akampata kwanza Simoni, ndugu yake, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake Kristo).
- Naye akamleta kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe ndiwe Simoni, mwana wa Yona;
- Kesho yake Yesu alitaka kutoka kwenda Galilaya, akamkuta Filipo, akamwambia, Nifuate.
- Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji wa Andrea na Petro.
- Filipo akamkuta Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye ambaye Mose aliandika habari zake katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, wa Nazareti.
- Nathanaeli akamwambia, Je! Filipo akamwambia, Njoo uone.
- Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akasema juu yake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.
- Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunijua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwa chini ya mtini, nilikuona.
- Nathanaeli akajibu, akamwambia, Rabi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu; wewe ndiwe Mfalme wa Israeli.
- Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? utaona mambo makuu kuliko haya.
- Akamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka, na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.