Biblia ya King James Version
Warumi, Sura ya 10:
- Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu na dua yangu nimwombayo Mungu kwa ajili ya Israeli ni kwamba waokolewe.
- Kwa maana nawashuhudia kwamba wana bidii kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.
- Kwa maana wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.
- Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.
- Kwa maana Musa anaandika juu ya haki ipatikanayo kwa sheria, ya kwamba mtu ayatendaye hayo ataishi kwa hayo.
- Lakini ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakayepanda mbinguni? (yaani, kumshusha Kristo kutoka juu;)
- Au, Ni nani atakayeshuka mpaka kilindini? (yaani, kumleta Kristo tena kutoka kwa wafu.)
- Lakini inasemaje? Neno li karibu nawe, katika kinywa chako na moyoni mwako, yaani, lile neno la imani tunalolihubiri;
- Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
- Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki; na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
- Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kila amwaminiye hatatahayarika.”
- Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani;
- Kwa maana, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.
- Basi watamwombaje yeye ambaye hawakumwamini? na watamwaminije yeye ambaye hawakusikia habari zake? nao watasikiaje pasipo mhubiri?
- Na watahubirije isipokuwa wametumwa? kama ilivyoandikwa, Jinsi ilivyo mizuri miguu yao waihubirio Injili ya amani, na kuhubiri habari njema ya mambo mema!
- Lakini si wote walioitii Injili. Kwa maana Isaya asema, Bwana, ni nani aliyeamini habari zetu?
- Basi imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Mungu.
- Lakini nasema, Je! Naam, sauti yao ilienea katika dunia yote, na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.
- Lakini nasema, Je! Israeli hawakujua? Kwanza Musa asema, Nitawatia ninyi wivu kwa watu wasiokuwa taifa, na kwa taifa la wapumbavu nitawakasirisha.
- Lakini Isaya ana ujasiri mwingi, na kusema, Nilipatikana na wale wasionitafuta; nalidhihirishwa kwa wale wasioniuliza.
- Lakini kwa Israeli asema, Mchana kutwa nimewanyoshea mikono watu wasiotii, wakaidi.