Kitabu cha Pili cha Yohana, Biblia ya Sauti Bila Malipo, Biblia ya King James Version katika Kiswahili

Biblia ya King James Version

Yohana wa 2, Sura ya 1:

  1. Mzee kwa bibi mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi tu, bali na wote walioijua hiyo kweli;
  2. Kwa ajili ya ile kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi milele.
  3. Neema na iwe kwenu, rehema na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo, Mwana wa Baba, katika kweli na upendo.
  4. Nalifurahi sana kwa kuwa nimeona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kutoka kwa Baba.
  5. Na sasa, mama, nakuomba, si kana kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.
  6. Na huu ndio upendo, kwamba tuenende kwa kuzifuata amri zake. Amri ndiyo hii, kama mlivyosikia tangu mwanzo, mwenende humo.
  7. Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili. Huyu ni mdanganyifu na mpinga Kristo.
  8. Jiangalieni ninyi wenyewe msije mkapoteza kazi tuliyofanya, bali tupate thawabu kamili.
  9. Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia.
  10. Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimsalimu;
  11. Kwa maana anayemsalimu anashiriki matendo yake maovu.
  12. Ninayo mengi ya kuwaandikia, sipendi kuandika kwa karatasi na wino;
  13. Watoto wa dada yako mteule wanakusalimu. Amina.