Biblia ya King James Version

2 Wathesalonike, Sura ya 2:

  1. Basi, ndugu, tunawasihi, kwa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa kukusanywa kwetu pamoja kwake;
  2. ili msitikisike upesi nia zenu, wala msitishwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka kana kwamba imetoka kwetu, kana kwamba siku ya Kristo imekaribia.
  3. Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote;
  4. Ambaye mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu au kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kwamba yeye ndiye Mungu.
  5. Je! hamkumbuki ya kuwa nilipokuwa pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
  6. Na sasa mnajua kinachozuia ili afunuliwe kwa wakati wake.
  7. Maana ile siri ya kuasi sasa inatenda kazi;
  8. Ndipo atakapofunuliwa yule Mwovu, ambaye Bwana atamwua kwa roho ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa mng’ao wa kuja kwake.
  9. hata yeye ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote na ishara na ajabu za uongo;
  10. na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
  11. Na kwa ajili hiyo Mungu atawaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;
  12. ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
  13. Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mnaopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewateua tangu mwanzo mpate wokovu, kwa kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;
  14. Hayo ndiyo aliyowaitieni kwa Injili yetu, mpate kupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.
  15. Kwa hiyo, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa neno au kwa waraka wetu.
  16. Basi, Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu, Baba yetu, aliyetupenda, akatupa faraja ya milele na tumaini jema, kwa neema;
  17. aifariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na kazi njema.