Biblia ya King James Version
2 Wathesalonike, Sura ya 2:
- Basi, ndugu, tunawasihi, kwa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa kukusanywa kwetu pamoja kwake;
- ili msitikisike upesi nia zenu, wala msitishwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka kana kwamba imetoka kwetu, kana kwamba siku ya Kristo imekaribia.
- Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote;
- Ambaye mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu au kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kwamba yeye ndiye Mungu.
- Je! hamkumbuki ya kuwa nilipokuwa pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
- Na sasa mnajua kinachozuia ili afunuliwe kwa wakati wake.
- Maana ile siri ya kuasi sasa inatenda kazi;
- Ndipo atakapofunuliwa yule Mwovu, ambaye Bwana atamwua kwa roho ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa mng’ao wa kuja kwake.
- hata yeye ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote na ishara na ajabu za uongo;
- na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
- Na kwa ajili hiyo Mungu atawaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;
- ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.
- Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mnaopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewateua tangu mwanzo mpate wokovu, kwa kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;
- Hayo ndiyo aliyowaitieni kwa Injili yetu, mpate kupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.
- Kwa hiyo, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa neno au kwa waraka wetu.
- Basi, Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu, Baba yetu, aliyetupenda, akatupa faraja ya milele na tumaini jema, kwa neema;
- aifariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na kazi njema.