Biblia ya King James Version
Mathayo, Sura ya 9:
- Akapanda chomboni, akavuka ziwa, akafika mjini kwao.
- Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala juu ya kitanda; Mwana, jipe moyo; umesamehewa dhambi zako.
- Na tazama, baadhi ya walimu wa Sheria wakasemezana wao kwa wao, Mtu huyu anakufuru.
- Naye Yesu akijua mawazo yao akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu?
- Kwa maana ni lipi lililo rahisi zaidi, kusema, Umesamehewa dhambi zako; au kusema, Inuka, uende?
- Lakini mpate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (ndipo akamwambia yule mwenye kupooza), Ondoka, ujitwike godoro lako, uende nyumbani kwako.
- Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake.
- Lakini makutano walipoona walistaajabu, wakamtukuza Mungu aliyewapa wanadamu uwezo wa namna hii.
- Yesu alipokuwa akipita kutoka huko alimwona mtu ameketi forodhani, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akainuka, akamfuata.
- Ikawa Yesu alipokuwa ameketi chakulani nyumbani, tazama, watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja naye na wanafunzi wake.
- Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?
- Yesu aliposikia akawaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.
- Lakini enendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si dhabihu; kwa maana sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi.
- Kisha wanafunzi wa Yohana wakamwendea wakisema, Mbona sisi na Mafarisayo hufunga mara nyingi, lakini wanafunzi wako hawafungi?
- Yesu akawaambia, Je! lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana-arusi, ndipo watakapofunga.
- Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu;
- Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; kama viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika;
- Alipokuwa akisema hayo, tazama, kiongozi mmoja akaja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa;
- Yesu akainuka, akamfuata pamoja na wanafunzi wake.
- Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake;
- Maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu vazi lake, nitapona.
- Yesu akageuka, akamwona, akasema, Jipe moyo mkuu, binti; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.
- Yesu alipofika nyumbani kwa yule liwali, akawaona wapiga vinanda na kundi la watu wakipiga kelele.
- Akawaambia, Ondokeni; kwa maana msichana hakufa, bali amelala. Nao wakamcheka kwa dharau.
- Lakini umati wa watu ulipotolewa, akaingia ndani, akamshika mkono, na yule msichana akasimama.
- Habari hizo zikaenea katika nchi ile yote.
- Yesu alipoondoka hapo, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele, wakisema, Uturehemu, Mwana wa Daudi.
- Naye alipofika nyumbani, wale vipofu walimwendea; Yesu akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia, Naam, Bwana.
- Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu na iwe kwenu.
- Macho yao yakafumbuliwa; na Yesu akawaonya kwa ukali, akisema, Angalieni mtu ye yote asijue.
- Lakini hao walipokuwa wakiondoka, wakaeneza habari zake katika nchi ile yote.
- Walipokuwa wakitoka, tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo.
- Na pepo alipotolewa, yule bubu akanena, makutano wakashangaa, wakisema, Haijapata kuonekana namna hii katika Israeli kamwe.
- Lakini Mafarisayo wakasema, Anawatoa pepo kwa mkuu wa pepo.
- Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masunagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya Ufalme wa Mungu, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
- Lakini alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.
- Kisha akawaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache;
- Basi mwombeni Bwana wa mavuno kwamba apeleke watenda kazi katika mavuno yake.