Biblia ya King James Version
Mathayo, Sura ya 21:
- Hata walipokaribia Yerusalemu, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, Yesu akawatuma wanafunzi wawili;
- Akawaambia, Nendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na mwana-punda pamoja naye;
- Na mtu akiwaambieni neno, mtasema, Bwana anawahitaji; na mara atawatuma.
- Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,
- Mwambieni binti Sayuni, Tazama, Mfalme wako anakuja kwako, mpole, naye amepanda punda, na mwana-punda, mtoto wa punda.
- Wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru.
- Wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo zao juu yao, wakampandisha juu yake.
- Umati mkubwa wa watu ukatandaza mavazi yao njiani; wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandaza njiani.
- Na makutano waliotangulia, na wale waliomfuata, wakapaaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi! Hosana juu mbinguni.
- Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Huyu ni nani?
- Umati wa watu ukasema, Huyu ni nabii Yesu wa Nazareti ya Galilaya.
- Yesu akaingia ndani ya hekalu la Mungu, akawafukuza wote waliokuwa wakiuza na kununua ndani ya hekalu, akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa;
- Akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
- Na vipofu na viwete wakamwendea hekaluni; naye akawaponya.
- Makuhani wakuu na walimu wa Sheria walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliokuwa wakipiga kelele Hekaluni wakisema, Hosana kwa Mwana wa Daudi! walikasirika sana,
- Wakamwambia, Wasikia hawa wasemavyo? Yesu akawaambia, Ndiyo; hamjapata kusoma, Kutoka katika vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa?
- Akawaacha, akatoka nje ya mji mpaka Bethania; akalala huko.
- Asubuhi na mapema alipokuwa akirudi mjini, aliona njaa.
- Akauona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; Na mara ule mtini ukanyauka.
- Wanafunzi walipouona walistaajabu, wakisema, Jinsi gani ule mtini umenyauka!
- Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia, Mkiwa na imani, wala msiwe na shaka, mtafanya si lile la mtini tu, bali hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka; ukatupwe baharini; itafanyika.
- Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.
- Naye alipoingia Hekaluni, makuhani wakuu na wazee wa watu wakamwendea alipokuwa akifundisha, wakamwuliza, Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? na ni nani aliyekupa mamlaka haya?
- Yesu akajibu, akawaambia, Nami nitawauliza neno moja;
- Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? kutoka mbinguni au kwa wanadamu? Wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, Tukisema, Yalitoka mbinguni; atatuambia, Mbona basi hamkumwamini?
- Lakini tukisema, Ilitoka kwa wanadamu; tunaogopa watu; kwa maana wote wanamwona Yohana kuwa nabii.
- Wakamjibu Yesu, wakasema, Hatujui. Naye akawaambia, “Nami sitawaambia ninyi ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani.”
- Lakini unafikiri nini? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo enenda ukafanye kazi katika shamba langu la mizabibu.
- Akajibu akasema, Sitaki, lakini baadaye akaghairi, akaenda.
- Akamwendea wa pili, akasema vivyo hivyo. Akajibu, akasema, Naenda, bwana;
- Je! ni yupi kati ya hao wawili aliyefanya mapenzi ya baba yake? Wakamwambia, Wa kwanza. Yesu akawaambia, Amin, nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.
- Kwa maana Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, nanyi hamkumwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini;
- Sikieni mfano mwingine: Palikuwa na mtu mmoja mwenye nyumba, aliyepanda shamba la mizabibu, akalizungushia ukuta, akachimba shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akalikodisha kwa wakulima, akaenda nchi ya mbali;
- Wakati wa matunda ulipofika, aliwatuma watumishi wake kwa wale wakulima ili wapokee matunda yake.
- Wale wakulima wakawakamata watumishi wake, wakampiga mmoja, wakamwua na mwingine wakampiga kwa mawe.
- Akatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza, wakawafanyia vivyo hivyo.
- Lakini mwisho kabisa akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu.
- Lakini wale wakulima walipomwona mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ndiye mrithi; njooni, tumuue, na tuutwae urithi wake.
- Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua.
- Basi, atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawafanya nini wale wakulima?
- Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale waovu, na shamba lake la mizabibu atawapa wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa majira yake.
- Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;
- Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lenye kuzaa matunda yake.
- Na mtu ye yote aangukaye juu ya jiwe hili atavunjika, lakini yeyote ambaye litamwangukia litamsaga.
- Makuhani wakuu na Mafarisayo waliposikia mifano yake walitambua kwamba alikuwa anawasema wao.
- Lakini walipotaka kumkamata, waliogopa umati wa watu kwa sababu walimwona kuwa nabii.