Biblia ya King James Version
Marko, Sura ya 9:
- Yesu akawaambia, Amin, nawaambia, wako baadhi ya hao wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu.
- Baada ya siku sita Yesu akawachukua Petro, Yakobo na Yohane juu ya mlima mrefu faraghani, naye akageuka sura mbele yao.
- Mavazi yake yakang’aa, meupe sana kama theluji; kwa maana hakuna dobi duniani awezaye kuwafanya weupe.
- Wakatokea Eliya pamoja na Musa, wakazungumza na Yesu.
- Petro akajibu, akamwambia Yesu, Mwalimu, ni vizuri sisi kuwa hapa; moja yako, na moja ya Musa, na moja ya Eliya.
- Maana hakujua la kusema; kwa maana waliogopa sana.
- Kukatokea wingu likawatia uvuli, na sauti ikatoka katika hilo wingu, ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, msikieni yeye.
- Mara walipotazama huku na huku, hawakumwona mtu yeyote ila Yesu peke yake pamoja nao.
- Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawakataza wasimwambie mtu ye yote waliyoyaona, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.
- Wakashika neno hilo wao kwa wao, wakiulizana wao kwa wao, maana ya kufufuka katika wafu.
- Wakamwuliza, wakisema, Mbona waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza?
- Akajibu, akawaambia, Eliya yuaja kwanza, na kurudisha yote; na jinsi ilivyoandikwa juu ya Mwana wa Adamu ya kwamba imempasa kupata mateso mengi na kudharauliwa.
- Lakini nawaambieni, Eliya amekuja, nao wakamtendea walivyotaka, kama ilivyoandikwa juu yake.
- Alipofika kwa wanafunzi wake, akaona umati mkubwa wa watu wakiwazunguka, na walimu wa Sheria wakijadiliana nao.
- Mara umati wote wa watu walipomwona walishangaa sana, wakamkimbilia kumsalimu.
- Akawauliza waandishi, Mnajadiliana nini nao?
- Mmoja katika ule umati wa watu akajibu, akasema, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu;
- na po pote amshikapo, humtoa machozi, na kutokwa na povu, na kusaga meno, na kuzimia; na hawakuweza.
- Akamjibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nitakaa nanyi hata lini? nitakuvumilia mpaka lini? mlete kwangu.
- Wakamleta kwake; naye alipomwona, mara yule pepo akamtia kifafa; akaanguka chini, akagaa-gaa akitokwa na povu.
- Akamwuliza baba yake, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utotoni.
- Na mara nyingi amemtupa motoni na ndani ya maji ili kumwangamiza;
- Yesu akamwambia, Ukiweza, yote yanawezekana kwake aaminiye.
- Mara babaye yule mtoto akapaza sauti, akasema kwa machozi, Ninaamini, Bwana; nisaidie kutokuamini kwangu.
- Yesu alipoona ya kuwa umati wa watu unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena.
- Yule pepo akapiga kelele, akamtia kifafa sana, akamtoka; hata wengi wakasema, Amekufa.
- Lakini Yesu akamshika mkono, akamwinua; naye akainuka.
- Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa?
- Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, ila kwa kusali na kufunga.
- Wakatoka huko, wakapita katikati ya Galilaya; wala hakutaka mtu ye yote ajue.
- Kwa maana alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akawaambia, Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa watu, nao watamwua; na akiisha kuuawa, atafufuka siku ya tatu.
- Lakini wao hawakuelewa neno hilo, wakaogopa kumwuliza.
- Yesu akafika Kapernaumu. Alipokuwa nyumbani, akawauliza, “Mlikuwa mnajadiliana nini njiani?”
- Lakini wakanyamaza; maana njiani walikuwa wakibishana ni nani aliye mkuu.
- Akaketi chini, akawaita wale Thenashara, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kuwa wa kwanza, atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote.
- Akamchukua mtoto mchanga, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia;
- Yeyote atakayempokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, ananipokea mimi;
- Yohana akamjibu, akasema, Mwalimu, tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi;
- Lakini Yesu akasema, Msimkataze, kwa maana hakuna mtu atakayefanya ishara kwa jina langu, awezaye kusema vibaya juu yangu.
- Kwa maana asiyepingana nasi yuko upande wetu.
- Kwa maana mtu ye yote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji kwa jina langu, kwa sababu ninyi ni wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake.
- Na ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutupwa baharini.
- Na mkono wako ukikukosesha, ukate;
- Ambapo funza wao hawafi, na moto hauzimiki.
- Na mguu wako ukikukosesha, ukate;
- Ambapo funza wao hawafi, na moto hauzimiki.
- Na jicho lako likikukosesha, ling’oe;
- Ambapo funza wao hawafi, na moto hauzimiki.
- Kwa maana kila mmoja atatiwa chumvi kwa moto, na kila dhabihu itatiwa chumvi.
- Chumvi ni nzuri; lakini chumvi ikiwa imepoteza ladha yake, mtaikolea nini? Iweni na chumvi ndani yenu, na muwe na amani ninyi kwa ninyi.